Serikali ya shirikisho imetangaza kuwa mafao ya jobseeker ya coronavirus, yataendelea kutolewa hadi mwisho wa Machi 2021 kwa kiwango cha chini.
Hisia mbali mbali zinendelea kutolewa Kenya, kufuatia madai kwamba ulaghai ulifanyika kwa ripoti ya maridhiano inayofahamika kama BBI, kwa kuingiza sehemu nyingine ambazo hazikuafikiwa na jopo maalum lililoandika ripoti hiyo.
Aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini, Godbless Lema, ambaye alishindwa katika uchaguzi wa mwezi uliopita baada ya kuhudumu kwa mihula miwili bungeni amekamatwa na anazuiliwa katika kaunti ya Kajiado nchini Kenya baada yake na familia kutoroka Tanzania na kuingia Kenya.