Waziri Mkuu Scott Morrison amesema mipango ya Victoria kufungua jimbo hilo, inaonesha kuna mwanga mwisho wa handaki kwa mwisho wa janga. Jimbo la Victoria limerekodi kesi mpya 1890 za maambukizi ya Covid pamoja na vifo vitano hii leo Jumapili 10 Oktobo, wakati 58% ya watu wenye zaidi ya miaka 16 wamepata chanjo kamili kwa sasa.
Kesi ya Ebola imethibitishwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kulingana na ripoti ya ndani Ijumaa kutoka kwenye maabara ya kitaifa ya matibabu, miezi mitano baada ya kumalizika kwa mlipuko wa hivi karibuni huko. Waziri wa afya wa Congo alikataa kuthibitisha habari hiyo, lakini akasema taarifa itachapishwa hivi karibuni. Haikujulikana mara moja ikiwa kesi hiyo inahusiana na mlipuko wa 2018 hadi 2020 ambao uliwaua zaidi ya watu 2,200 mashariki mwa nchi hiyo au mlipuko uliowaua watu sita mwaka huu.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anasema nchi yake itarudisha kazi za sanaa 26 za Kiafrika nchini Benin baadaye mwezi huu. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anasema nchi yake itarudisha kazi za sanaa 26 za Kiafrika nchini Benin baadaye mwezi huu. Majadiliano yamekuwa yakiendelea kwa miaka kadhaa juu ya kurudisha kazi za sanaa kutoka kwa Ufalme wa Dahomey wa karne ya 19.