Taarifa ya Habari 10 Oktoba 2023

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Maandamano yakupinga Israel yameshuhudiwa mjini Sydney wakati wa makabiliano kati ya jeshi la Israel na Hamas yakiendelea, wakati huo huo mjini Perth, kundi linalo unga mkono Israel limeshiriki katika ibada maalum kwa niaba ya nchi hiyo.


Wana harakati wanao omba kuundwa kwa sauti yawa Australia wa kwanza bungeni, wana ongeza juhudi za kampeni zao katika siku za mwisho kabla ya kura ya maoni ya Jumamosi. Matokeo ya kura mpya za maoni yanaonesha kuwa kampeni ya La, bado ina uvutio mkubwa kuliko kampeni ya Ndio.

Makombora yalianguka katika hospitali ya Al-Nau mjini Omdurman, mji pacha wa mji mkuu wa Sudan Khartoum, chanzo cha afya kimeliambia shirika la habari la AFP kwa njia ya simu. Takriban raia watatu waliuawa siku ya Jumatatu nchini Sudan wakati makombora yaliposhambulia hospitali muhimu katika mji mkuu, chanzo cha afya kimesema wakati mapigano kati ya majenerali hasimu yakiendelea bila ya kupungua.

Maofisa wa polisi nchini Uganda na wenzao wa jeshi, wameripotiwa kuweka vizuizi katika afisi kuu za chama cha upinzani cha National Unity Platform (NUP), kinachoongozwa na mwanasiasa wa upinzani Bobi Wine. Katika taarifa yake kwenye mtandao wa X, chama hicho kimethibitisha kuzuiliwa kwa afisi zake katiaka eneo la Kamwokya. Wiki iliyopita, polisi walimsindikiza Bobi Wine hadi nyumbani kwake baada ya kurejea Uganda kutoka Afrika Kusini, wakisema kuwa hatua hiyo ilikuwa ni kumzuia kuandaa maandamano.


Wanaume barani Afrika wametakiwa kuwa mstari wa mbele kupambana na vitendo vya ukeketetaji wa wanawake wakati serikali katika bara hilo zimeombwa kuanzisha mitaala inayofundisha madhara ya ukeketaji kuanzia shule za msingi. Wadau waliohudhuria mkutano wa pili wa kimataifa kuhusu kutokomeza ukeketaji wa wanawake, uliofanyika jijini Dar es salaam, wamesema utolewaji kwa mapana wa elimu kuhusu madhara ya ukeketaji ndiyo suluhisho sahihi litakalotokomeza vitendo hivyo barani Afrika.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Taarifa ya Habari 10 Oktoba 2023 | SBS Swahili