Taarifa ya Habari 11 Aprili 2023

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Kaimu Waziri Mkuu Penny Wong, na waziri wa biashara Don Farrell, wame thibitisha kuwa serikali ya shirikisho imefikia maafikiano na Beijing, kwa suluhu ya mgogoro wakibiashara wa shayiri.


Mamlaka wana wahamasisha wakaazi wa Magharibi Australia wajiandae kwa siku zijazo, wakati upepo mkali na mvua nzito zimetabiriwa kwa sehemu za kusini ya jimbo hilo. Ofisi ya utabiri wa hewa imeonya kuwa upepo unaweza fika kasi ya 200km/h, wakati kimbunga cha kitengo cha nne kina elekea katika pwani ya Kimberley. Mafuriko yanatarajiwa pia katika sehemu za Great Northern Highway, mililita 200 ya mvua ikitarajiwa kunyesha katika bonde la mto De Grey.

Msemaji wamaswala yawa Australia wakwanza katika upinzani wa shirikisho Julian Leeser, amejiuzulu kwa sababu ya upinzani wa chama cha Liberal kwa pendekezo la Sauti yawa Australia wa kwanza Bungeni. Chama hicho kiliamua wiki jana kupinga pendekezo hilo, ambalo litapigiwa kura katika kura ya maoni kitaifa baadae mwaka huu.

Jumanne Aprili 11 ni miaka 4 tangu mapinduzi ya Sudan kufanyika, na kupelekea jeshi kumuondoa madarakani Rais Omar al Bashir. Kufikia sasa matumaini ya kujipatia utawala wa kiraia hayajatimia, huku. vuguvugu la kuitisha demokrasia nchini humo likiwa kwenye mvutano na jeshi kuhusu utawala.

Serikali ya Kenya imekiri kwamba inakabiliwa na uhaba wa pesa ambao umechelewesha malipo ya mishahara ya maelfu ya wafanyikazi wa umma. Vyama viwili vinavyowakilisha wafanyikazi wa serikali ya kitaifa na kaunti vimetoa notisi za nia yao ya kususia kazi.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service