Serikali ya shirikisho inaongeza msaada kwa watoto ambao wako katika mazingira magumu kupata huduma ya meno, kwa kuwekeza kwa mfumo wa mafao ya meno kwa miaka mingine minne. Ratiba yakitaifa ya mafao ya meno ya watoto, itaruhusu watoto wanao stahiki wenye umri wa kati ya miaka 0-17, kupata $1,026 kwa mafao kwa muda wa miaka mbili kwa huduma ya msingi ya meno, itakayo tolewa katika sekta za umma na binafsi.
Chanjo ya virusi vya Ebola aina ya Sudan ni moja kati ya chanjo tatu zilizopendekezwa kufanyiwa majaribio na jopo huru la wataalamu wa WHO. Chanjo nyingine mbili zitaongezwa kwenye majaribio wakati dozi zitakapowasili. Shirika la afya duniani (WHO) limesema kuwasili kwa moja ya chanjo tatu za majaribio ya Ebola nchini Uganda hapo alhamisi "kunaashiria hatua muhimu ya kihistoria katika uwezo wa kimataifa wa kukabiliana na milipuko". Dozi 1,200 za chanjo ya virusi vya Ebola aina ya Sudan ziliwasili siku 79 tu baada ya mlipuko kutangazwa Septemba 20, WHO ilisema.
Katika kambi ya wakimbizi Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC) Eric, Samuel, Tuyisenge na Florence walielezea yaliyowasibu walipotembea maili kadhaa wakikimbia shambulizi baya la waasi katika kijiji chao. Waasi wa M23 waliwaua raia wasiopungua 131 wakiwemo watoto 12 na walifanya ubakaji zaidi ya dazeni mbili hapo Novemba 29-30 katika vijiji viwili kwenye eneo la Rutshuru, ikiwa ni pamoja na Kishishe, Umoja wa Mataifa unasema.