Taarifa ya Habari 11 Julai 2023

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Australia na Ujerumani zatia saini ya biashara huru naku ahidi misaada ya ziada kwa Ukraine.


Mhakiki huru ameteuliwa kuchunguza uwezekano wa ukiukwaji wa kanuni za maadili chini ya mfumo wa robodebt. Steve Sedgwick atachunguza ukiukwaji wa kanuni na wafanyakazi wa umma wanao ungwa na mradi huo.

Utafiti mpya umebaini kuwa wapangaji jimboni Qld, Kusini Australia na NSW wanakabiliana na changamoto nyingi za gharama kote nchini. Utafiti huo uliofanywa na kampuni ya utafiti Suburbtrends ya jimbo la NSW, umedokeza kuwa Qld inakabiliana na shinikizo kubwa zaidi katika mamlaka yoyote wakati gharama za kodi zime ongezeka kwa 16% katika mwaka uliopita.

Serikali ya Sudan Jumatatu ilikataa kushiriki katika mkutano wa kikanda wenye lengo la kumaliza miezi mitatu ya mapigano ya kikatili, ikiishtumu Kenya ambayo inasimamia mazungumzo hayo, kukipendelea kikosi hasimu cha wapiganaji.

Macho ya Wakenya sasa yanamuelekea Jaji Mkuu Martha Koome, anayetarajiwa kupokea faili ya kesi kuhusu Sheria ya fedha ya mwaka 2023. Jumatatu, Julai 10, 2023, Jaji Mugure Thande aliendeleza marufuku ya utekelezaji Sheria hiyo iliyopaswa kuanza Julai 1. Kesi hiyo iliwasilishwa na Seneta wa Busia, Okiya Omtatah.


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service