Chama cha The Greens kime sema serikali ya Albanese "inakataa kutingika" katika mashauriano kuhusu mfuko wao wa Housing Australia Future Fund. Mjadala kati ya vyama hivyo viwili uta anza tena wiki ijayo ndani ya seneti, ambako chama cha Greens kinatumai kupata makubaliano kwa kusitishwa kwa muda kwa ongezeko ya kodi za nyumba pamoja na uwekezaji wa ziada kwa nyumba za bei nafuu.
Wakazi wameripoti hali ya utulivu katika mji mkuu wa Sudan Khartoum Jumamosi tangu kuanza kutekelezwa makubaliano ya kusitisha mapigano kwa saa 24 kati majenerali wawili wanaopigana, lakini watu wachache wanaamini kuwa sitisho la mapigano litadumu.
Watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Kiislamu waliwaua watu 12 kuho mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Alhamisi jioni, kulingana na maafisa wa wilaya ya Beni katika jimbo la kivu Kaskazini.
Hatimae Pep Guardiola, iongoza Manchester City kupata ubingwa wa klabu bingwa barani Ulaya.