Taarifa ya Habari 11 Septemba 2022

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Mfalme Charles III ametangazwa rasmi kama kiongozi mpya ya Australia, katika sherehe maalum ndani ya Bunge la Taifa mjini Canberra.


Kifo cha Malkia akiwa na umri wa miaka 96, kimezua mjadala mpya kuhusu uwezekano wa Australia kuwa Jamuhuri. Swala hilo liliwasilishwa kwa wapiga kura miaka 23 iliyopita, nakukataliwa kati ya utata kuhusu swali lililo ulizwa.

Waziri wa Sheria wa Jamhuri ya Kidemkorasia ya Kongo anasema Uganda imeanza kuilipa Kinshasa fidia ya dola milioni 65 kati ya 325 kama ilivyoamriwa na Mahakama ya Sheria ya Kimataifa ICJ.Kiwango hicho cha fedha ni kidogo sana kulingana na dola bilioni 11 ambazo DRC imekua ikidai, ingawa Uganda imeichukulia hukumu hiyo haikuwa ya haki, na wamesikitishwa kwamba uamuzi ulichukuliwa wakati nchi hizo mbili zilikuwa zinaendelea kuimarisha uhusiano kati yao.

Rwanda huenda itaisaidia Benin kwa msaada wa uchukuzi ili kuweza kukabiliana na uasi unaongezeka unaofanywa na wanamgambo wa kiislamu, ambao unatishia kanda zima ya Afrika Magharibi. Hii ni kulingana na msemaji wa rais ya Benin, Wilfried Leandre Houngbedji. Akizungumza na shirika la habari la Reuters, Hougbedji amesema mazungumzo kati ya nchi yake na Rwanda yanaendelea kuhusu uwezekano wa kupata msaada wa kijeshi bila ya kuwahusisha wanajeshi wa Rwanda.


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service