Taarifa ya Habari 12 Julai 2022

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Kongamano la ajira la serikali linatazamia wahamiaji, wajaze mapengo mhimu ya kazi ila mweka hazina amesema hiyo siyo suluhu pekee.


Tume huru dhidi ya ufisadi ya New South Wales almaarufu ICAC, inatarajia kuchunguza kilicho sababisha kazi yakifahari ya biashara, kutolewa kwa naibu kiongozi wa zamani wa NSW John Barilaro. Kamati ya nyumba ya juu bungeni kwa sasa inafanya uchunguzi kwa utoaji wa kazi hiyo, na imetuma ushahidi kutoka mgombea wa ajira aliye pendelewa wa kwanza Jenny West, kwa tume hiyo ya I-C-A-C.

Kampeni mpya yakitaifa dhidi ya ubaguzi wa rangi imezinduliwa na, inawaomba wa Australia ambao hawapitii uzoefu wa ubaguzi wa rangi, watafakari sababu na madharayake na wafanye mengi zaidi kuishughulikia. Kampeni hiyo yamatangazo kwenye majukwaa mengi, inalengo lakujenga uelewa kwa jinsi ubaguzi wa rangi hutokea kwa kiwango cha mfumo na mtu kw amtu na, matumaini nikuwapa watu vifaa vyaku itambua nakuishughulikia.

Polisi wa Uganda walifyatua gesi ya kutoa machozi na kukamata darzeni ya waandamanaji Jumatatu baada ya maandamano ya kupinga kupanda kwa bei ya chakula na mafuta ambayo yaligeuka vurugu. Taifa hilo la Afrika mashariki lenye watu milioni 45 linakabiliwa na mdororo wa uchumi uliochochewa na janga la Covid 19, na hali hiyo ikazidi kuwa mbaya zaidi kutokana na vita vya Russia nchini Ukraine. Jumatatu, waandamanaji walichoma matairi na kufunga barabara kuu yenye shughuli nyingi huko Jinja, umbali wa kilomita 80 mashariki mwa mji mkuu Kampala, wakiomba serikali kutoa ruzuku ya chakula kinachotumiwa sana.


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Taarifa ya Habari 12 Julai 2022 | SBS Swahili