Kashfa ya robodebt yawafikisha mawaziri na waziri mkuu wazamani mbele ya tume yakifalme kujieleza. Na muaustralia wa mwaka na mtetezi wa ulemavu Dylan Alcott, ameomba pawe elimu zaidi kuhusu ufikiaji na ushirikishwaji katika nguvu kazi.
Marekani imetangaza msaada wa dola bilioni 55 kwa nchi za Afrika, ndani ya kipindi cha miaka mitatu ijayo. Tangazo hilo limetolewa wakati rais Joe Biden akijitayarisha kuwa mwenyeji wa viongozi wa nchi za Afrika, mjini Washington DC. Biden atafanya majadiliano na kundi dogo la viongozi wa Afrika kuhusu chaguzi zitakazofanyika mwaka 2023 na demokrasia barani Afrika.
Bunge la Afrika Kusini linatarajiwa kufanya kikao maalum kushughulikia ripoti ya jopo la wataalam wa kisheria ambao wamegundua kuwa Rais Cyril Ramaphosa anaweza kuwa amevunja kiapo chake. Hii ni kuhusiana na kashfa ya suala la shamba inayomzunguka rais, ambapo Bwana Ramaphosa ameshtakiwa kwa kuficha wizi wa sarafu za kigeni katika shamba lake la kibinafsi mnamo 2020. Hata hivyo, Bwana Ramaphosa amekanusha mara kwa mara makosa yoyote.