Taarifa ya Habari 13 Juni 2023

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Waziri Mkuu Anthony Albanese amesema Australia inastahili chukua fursa yakuwa kiongozi wa nishati mbadala.


Bw Albanese alizungumza katika kongomano la taifa la kamati ya uchumi na maendeleo ya Australia [[CEDA]] mjini Canberra. Hotuba yake ili lenga fursa ya Australia kuibuka kama nguvu kubwa nduniani, inapokuja swala la suluhu la nishati yakibichi na kwa mgogoro wa mazingira.

Chama cha The Greens kime kataa makubaliano ya chama cha Labor kwa mfuko wa nyumba wenye thamani ya $10 bilioni, wakati muda tata unakaribia kwa sera mhimu ya uchaguzi ya serikali ya shirikisho. Wakati chama cha mseto kimekataa kupigia sera hiyo kura, serikali ya Albanese inategemea msaada wa wabunge huru na vyama vidogo.

Mashtaka zaidi yanatarajiwa kufunguliwa dhidi ya dereva anaye shtumiwa kwa kuwajibika kwa moja ya ajali baya zaidi ya barabarani nchini Australia, ambayo iliwauwa wageni 10 wa harusi pamoja naku wajeruhis madazeni zaidi.

Rais wa Kenya William Ruto ameapa Jumatatu kuandaa mkutano wa ana kwa ana, kati ya majenerali wanaohasimiana nchini Sudan ili kumaliza mzozo unaolikumba taifa hilo baada ya makubaliano kadhaa ya kusitisha mapigano kushindwa kufanyika, ofisi ya rais wa Kenya imesema.

Wanamgambo wenye silaha wa kundi la CODECO wameshambulia kambi ya wakimbizi katika jimbo la Ituri na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40 Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Taarifa hizo zimetolewa leo na Richard Dheda afisa tawala wa huko Bahema Badjere eneo la Djugu. Mwakilishi wa mashirika ya kiraia Desire Malodra amesema wanamgambo hao walianza kufyatua risasi na watu wengi waliteketea kwa moto katika nyumba zao huku wengine wakiuawa kwa mapanga.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Taarifa ya Habari 13 Juni 2023 | SBS Swahili