Takriban tani 1,100 ya taka ime ondolewa kutoka mto Brisbane, wiki mbili baada ya mji huo kufurika. Mweka hazina wa Queensland, Cameron Dick amesema mamlaka wanarejesha bandari ya Brisbani, taratibu katika hali yake yakawaida ya kazi.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta Jumamosi alimuidhinisha rasmi mpinzani wake wa zamani wa kisiasa kushika wadhifa wa juu zaidi wa nchi hiyo, Raila Odinga, wiki kadhaa baada ya vyama vyao kuungana pamoja kabla ya uchaguzi wa rais na bunge wa mwezi Agosti mwaka huu. Tangazo hilo lilijiri baada ya naibu wa Rais wa nchi hiyo William Ruto, ambaye pia ana nia ya kugombea kiti cha urais, kutimuliwa kutoka kwa chama cha Jubilee. Ruto, aliyehamia chama cah United Democratic Alliance, UDA, anatajwa na wachambuzi kama mpinzani mkuu wa Odinga, kwelekea kwa uchaguzi wa mwezi Agosti.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) linaripoti ukame nchini Somalia unasababisha mzozo wa kibinadamu na ukosefu wa makazi. UNHCR inasema maelfu ya watu wanakimbia maeneo yenye ukame wakitafuta ardhi yenye rutuba na misaada ya kibinadamu ili kuweza kujinusuru kimaisha.