Taarifa ya Habari 13 Novemba 2022

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Serikali ya shirikisho kuendelea kuwinda nakuvuruga shughuli za wahalifu wa mtandaoni asema waziri usalama wa mtandaoni


Serikali ya New South Wales imesema itatafuta msaada kutoka ng'ambo, kupiga jeki jibu lake kwa hali ya dharura inayo endelea ya mafuriko. Baadhi yamaeneo ya jimbo hilo yanaweza pokea hadi mililita 150 ya mvua hii leo Nov 13. Maeneo yanayo zua wasiwasi zaidi nikama; Wagga, Albury, Yass, Young na miji yote ambayo iko karibu ya mto Murray.

Maelfu ya nyumba na biashara mjini Adelaide huenda zikasalia bila umeme hadi jumanne, baada ya dhoruba kali kugonga mji huo. SA Power imesema kuwa dhoruba hiyo ilikuwa na nguvu sana kiasi kwanga ilisababisha zaidi ya maeneo 310 kupoteza umeme pamoja nakuangusha takriban miamba 500 ya umeme. Kampuni hiyo imeomba msaada kutoka washirika wake katika majimbo mengine nchini, kwa ajili yakusaidia kurejesha umeme katika maeneo yaliyo athiriwa.

Wanajeshi wa Kenya wamewasili Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa ajili ya kupambana na makundi ya waasi ambayo yamesababisha ukosefu wa usalama katika eneo hilo kwa miongo kadhaa. Wanajeshi 903 wa Kenya wameingia DRC chini ya makubaliano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kuna zaidi ya makundi ya waasi 120 mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, ambayo yamekuwa yakishambulia raia, kusababisha vifo na uharibifu wa mali.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service