Kiongozi wa upinzani Peter Dutton amesema ushindi wa kampeni ya 'La' katika kura ya maoni ya sauti yawa Australia wa kwanza bungeni kesho, haita kuwa kukataliwa kwa mahitaji yawa Australia wa kwanza. Bw Dutton pamoja na wanao unga mkono kampeni ya 'La' wanafashan kampeni za dakika ya mwisho, kabla wa Australia waingie debeni kesho kutoa hukumu zao. Kwa upande wake Waziri Mkuu Anthony Albanese ana wahamasisha wa Austrlaia waunge mkono Sauti ya waAustralia wa kwanza bungeni, kama sehemu ya kampeni za mwisho kabla vituo vyakupiga kura vifunguliwe rasmi kesho. Kampeni ya 'Ndio' imesema Sauti ni mhimu kwa kushughulikia tofauti kubwa katika sehemu kama afya na matokeo yakiuchumi kati yawa Australia wa kwanza na wa Australia wenza.
Wanajeshi wanane wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa waliokuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamewekwa kizuizini kwa madai ya unyanyasaji wa kijinsia. Chanzo cha Umoja wa Mataifa na chanzo cha usalama cha Congo vilisema madai hayo yanawahusu walinda amani wanane wa Afrika Kusini waliokuwa katika mji wa Mashariki wa Beni. Vyanzo hivyo viwili vilizungumza kwa sharti la kutotajwa majina kwa sababu hawakuruhusiwa kulijadili suala hili na vyombo vya habari.
Serikali ya Rwanda inajaribu kuwanyamazisha wakosoaji na wapinzani wanaoishi nje ya nchi kupitia mauaji holela, utekaji nyara na vitisho, kulingana na ripoti ya Human Rights Watch. Ripoti hiyo inaelezea kuwa Rais wa Rwanda Paul Kagame na chama chake tawala cha Rwandan Patriotic Front, au RPF, mara nyingi wanasifiwa kwa kuijenga upya na kuiunganisha nchi hiyo baada ya mauaji ya kimbari ya 1994.
Mahakama ya Kenya Alhamisi ilitupilia mbali kesi ya kupinga uamuzi wa serikali wa kuruhusu uingizaji na kulima mazao yaliyofanyiwa mabadiliko ya kijenetiki ili kusaidia kukabiliana na tatizo la chakula. Oktoba mwaka jana serikali iliondoa marufuku ya muongo mmoja kwa mazao ya GMO ili kukabiliana na kupungua kwa usalama wa chakula kufuatia ukame mbaya sana kulikumba eneo la Pembe ya Afrika katika miaka 40.