Jeshi la mapinduzi nchini Mali limeapa kuunda serikali ya mpito ya muda wa miezi 18 ili kuirejesha nchi hiyo katika utawala wa kiraia baada ya mapinduzi ya mwezi uliopita dhidi ya serikali ya rais Ibrahim Boubacar Keita lakini viongozi maarufu wamekataa kuendelea kwa ushawishi wa kijeshi nchini humo.
Waokoaji wanachimba vifusi kufuatia kuporomoka kwa mgodi wa dhahabu nchini DR Congo na kuwawacha watu takriban 50 wakiwa wamefariki. Mgodi huo uliopo karibu na mji wa Kamituga , mashariki mwa taifa hilo uliporomoka siku ya ijumaa kufuatia mvua kubwa.
Viongozi wa Tanzania na Uganda hatimaye wamekubaliana kuhusu ujenzi wa bomba la mafuta linalotarajiwa kujengwa kutoka mji wa Hoima nchini Uganda hadi changalieni mjini Tanga Tanzania.