Utafiti mpya wawatumiaji umedokeza kuwa watu wanakaza mikanda zaidi, kama sehemu ya jibu kwa ongezeko ya viwango vya riba pamoja na ongezeko kwa ujumla ya gharama ya maisha. Kwa mujibu wa benki yamadola, matumizi ya nyumba yaliongezeka kwa asilimia 0.8 katika mwezi wa Agosti.
Wanamgambo wa Tigray nchini Ethiopia walisema Jumapili wako tayari kwa usitishaji mapigano na watakubali mchakato wa amani unaoongozwa na Umoja wa Afrika, kuondoa kikwazo katika mazungumzo na serikali ili kumaliza karibu miaka miwili ya vita vya kikatili. Serikali ya Ethiopia hapo awali ilisema iko tayari kwa mazungumzo yasiyo na masharti "wakati wowote, mahali popote," yaliyosimamiwa na AU yenye makao yake makuu mjini Addis Ababa.
Rais mteule wa Kenya, William Ruto, ataapishwa hivi leo Jumanne kama rais wa taifa hilo la Afrika Mashariki. Hafla ya uapisho itafanyika katika uwanja wa kimataifa wa michezo wa Kasarani, nje kidogo ya mji mkuu, Nairobi. Kwa mujibu wa katiba ya Kenya, rais mtele ni lazima aapishwe kati ya Saa nne asubuhi na saa nane mchana. Jumatatu, Dr Ruto alikutana na rais anayeondoka madarakani, Uhuru Kenyatta katika ikulu mjini nairobi, huku mchakato wa kukabidhiana mamlaka, ulioanza Jumanne wiki jana ukiendelea.