Mamepa hii leo watu waliondolewa katika uwanja wa ndege wa Canberra, baada ya ripoti za milio ya risasi kusikika katika sehemu ambako abiria hupumzika wakisubiri kuabiri ndege. ACT Police imesema mwanaume mmoja alikamatwa katika sehemu la tukio na bunduki kuchukuliwa, na mtu ambaye amekamatwa ina aminiwa kuwa ndiye mtu pekee anaye wajibika kwa tukio hilo.
Meli ya kwanza ya nafaka inayoelekea barani Afrika kutoka nchini Ukraine tangu uvamizi wa Russia mwezi Februari mwaka huu ilitia nanga katika bandari ya Pivdennyi, jana Ijumaa, waziri wa miundombinu wa Ukraine alisema.
Wakenya wanaendelea kusubiri matokeo rasmi ya uchaguzi wa rais kutoka kwa tume ya uchaguzi na mipaka ya nchi hiyo, IEBC, siku tano baada ya kushiriki zoezi la kumchagua rais, magavana, wabunge na wawakilishi wengine. Hii ni kufuatia uchaguzi uliofanyika Jumanne wiki hii katika taifa hilo la Afrika Mashariki.Hii ni kufuatia uchaguzi uliofanyika Jumanne wiki hii katika taifa hilo la Afrika Mashariki.