Bi Bullock kwa sasa ndiye Naibu Gavana wa Benki Kuu, na alianza kufanya kazi katika benki hiyo mnamo mwaka wa 1985. Ata chukua usukani wa benki hiyo Septemba 18, hatua ambayo italeta kikomo cha uongozi wa miaka saba wa Philip Lowe. Waziri Mkuu Anthony Albanese amesema uteuzi wa Bi Bullock unafuata mchakato mgumu ulio jumuisha mashauriano na upinzani.
Watoto wanaporejea shuleni nchini Australia, maafisa wa afya wamezua wasiwasi kuhusu viwango vidogo vya wanao chukua chanjo za mafua. Imeripotiwa ni 35% ya watoto ndiwo wame chanjwa kitaifa.
Msichana wa miaka 11 alifariki katika hospitali moja ya Qld kupitia kirusi hicho, hicho ni kifo cha pili cha mtoto ambacho kimethibitishwa kwa sababu ya mafua katika wiki iliyopita.
Profesa Kristine McCartney ni Mkurugenzi wa Kituo cha taifa cha chanjo, utafiti na ufuatiliaji, yeye pia ni daktari wa watoto. Prof McCartney ame eleza shirika la habari la Seven Network kwamba, aina hii ya kirusi cha mafua inasababisha ugonjwa mbaya.
Serikali ya Kenya jana Alhamisi ilisema takribani watu kumi, walifariki na zaidi ya 300 akiwemo mbunge mmoja wamekamatwa kufuatia maandamano yaliyoitishwa na mkuu wa upinzani Raila Odinga yakipinga serikali ya rais William Ruto. Maandamano hayo yaliyofanyika Jumatano ikiwa ni ya pili katika kipindi cha wiki moja, yalizua ghasia na kusababisha hasara na kusitisha biashara katika miji mikubwa ambako maandano yamekuwa yakifanyika.
Ruto, Alhamisi, aliuonya upinzani kuwa hawezi kutishwa na matukio ya uharibifu wa mali ya umma, vurugu, ghasia na rabsha zinazoondoa utulivu wa nchi huku akimshtumu Raila Odinga kwa kuivuruga serikali yake. Mara kwa mara, rais Ruto amekuwa akiulaumu utawala wa rais mstaafu Uhuru Kenyatta kwa matatizo ya kiuchumi ya Kenya. Akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi baada ya Ruto, Odinga ametangaza kuwa wiki ijayo upinzani utaandaa duru ya tatu ya maandamano.
Wanasiasa wawili muhimu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Martin Fayulu na Joseph Kabila, wametangaza kutowania urais kwenye uchaguzi wa Disemba wakidai kuwa tume ya uchaguzi inaendesha mchakato usio wa kidemokrasia. Miongoni mwa madai waliyoyatowa walipokutana na mkuu wa CENI, Denis Kadima, siku chache zilizopita, upinzani ulisisitiza kuwa daftari la uchaguzi likaguliwe na kampuni huru yenye umaarufu na ujuzi wa kimataifa, lakini CENI iliyatupilia mbali masharti hayo.
Na aina mpya ya vitunguu ambavyo havitozi machozi, vita achiwa sokoni katika jaribio la kwanza nchini Australia.
Kitunguu hicho chakipekee cha rangi ya kahawai, kime undwa kwa miongo kikiwa na kemikali chache ambazo hufanya watu walie wanapo kikata.
Masoko ya Woolworths ambayo yako NSW, Victoria na ACT, yata uza vitunguu hivyo ambavyo vimepewa jina la "Happy Chop Tearless Onions" kuanzia hivi sasa hadi September.
Katika michezo,
Timu ya AFL ya Sydney Swans, ime ibuka mshindi baada yakupewa ushindani mkali kutoka timu ya Western Bulldogs, Swans wame shinda mechi hiyo kwa alama 78 kwa 76.
Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya mechi hiyo kuisha, mwalimu wa Sydney Swans John Longmire alisema huo ulikuwa ushindi mzuri katika mechi yake ya 300 akiwa mwalimu.
Na zimesalia siku 6, kwa mechi ya kwanza ya kombe la dunia la mchezo wa mpira wa miguu wa wanawake kuanza nchini Australia na New Zealand. New Zealand itakabiliana na Norway katika mechi ya kwanza na muda mfupi baadae, Australia ita ikaribisha Ireland dimbani.