Polisi walishambuliwa kwa chupa wakati wa makabiliano kati yao na mamia ya waandamanaji mjini London, ambao walipuuza agizo la kutoshiriki maandamano.
Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema waliojifunza kutokana na milipuko ya awali ya Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ni tiba muwafaka ziliruhusu kupata udhibiti wa haraka wa ugonjwa huu ambao unasababisha vifo katika jimbo la Equateur.
Changamoto ya kupata taarifa nchini Burundi baada ya kifo cha ghafla cha Rais Pierre Nkurunziza kilichotokea Juni 8, kinaendelea kudidimiza mazingira ya vyombo vya habari baada ya kukandamizwa kwa miaka kadhaa.