Kaimu kiongozi wa jimbo la Victoria, amesema ni vizuri kuona kiongozi wa jimbo hilo Daniel Andrews akihamishwa kutoka kitengo cha wagonjwa mahtuti nakupelekwa katika chumba kingine cha wagonjwa hospitalini. Bw Andrews alitereza kwenye ngazi zilizo kuwa na mji mapema mwezi huu, nakunja mbavu kadhaa pamoja nakupata jeraha katikati ya uti wa mgongo wake.
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amekanusha habari zilizoenea kwa karibu wiki nzima sasa kwamba Rais John Magufuli ni mgonjwa, akisema kuwa rais “ni mzima na anaendelea na kazi zake kama kawaida”. Majaliwa ambaye alikuwa akizungumza wakati wa sala ya Ijumaa mjini Njombe, kusini mwa Tanzania aliwataka Watanzania kupuuza ripoti zinazosambaa ambazo zinaeleza kuwa kiongozi wao ni mgonjwa.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeahirisha kampeni ya chanjo ya AstraZeneca dhidi ya Covid-19, ikifuata mfano wa nchi nyingine kadhaa zilizochukua kama hiyo. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya serikali ya nchi hiyo. Serikali ya nchi hiyo ilipokea dozi milioni 1.7 ya chanjo hiyo inayotengenezwa na kampuni ya AstraZeneca ya Uingereza na Sweden, na ilitarajiwa kuanza zoezi la kuwachanja watu Jumatatu ya tarehe 15 Machi.