Meya wa mji wa Brisbane ame ahidi kuwekeza $1 milioni, kusaidia kugeuza kifaa cha karantini kuwa makaazi ya dharura ya wasio na mwakaazi. Meya Adrian Schrinner amesema uwekezaji huo kutoka bajeti ya halmashauri ya jiji, utaelekezwa kwa vifaa vya kufulia katika eneo la Pinkenba lenye vitanda 500, pamoja na usafiri na huduma za maktaba.
Kifaa cha kupandikiza mioyo ya watoto, kime anzishwa jimboni New South Wales. Kiongozi wa NSW Chris Minns ametoa tangazo hilo nje ya hospitali ya watoto ya Westmead, ambako mradi huo uta simamiwa.
Jeshi la Sudan linalopigana na kikosi cha RSF watarejea kwenye meza ya mazungumzo siku ya Jumapili, mwanadiplomasia mwandamizi wa Saudia Arabia alisema hayo huku mashambulizi ya anga na mapigano makali yakiendelea usiku kucha kuzunguka Khartoum licha ya makubaliano ya kuwalinda raia.
Wachunguzi nchini Kenya wamefukua miili mingine 29 siku ya Ijumaa na kufanya idadi ya waathirika wanaohusishwa na ibada ya kutokula wakiamini siku ya kiama imekaribia kufikia 179, ambapo wengi wao ni watoto.