Taarifa ya Habari 14 Novemba 2021

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Queensland yatimiza lengo mhimu la utoaji wa chanjo ya UVIKO-19 na upinzani waikosoa serikali ya shirikisho kwa juhudi zake zakukabiliana na kupunga uzalishaji wa hewa chafu.


Chama cha Greens kime elezea maafikiano ya mwisho ya mkutano wa COP26 kama kukataliwa kwa serikali ya shirikisho ya Australia. Chini ya maafikiano hayo, viongozi wata alikwa tena kushiriki katika mkutano wa umoja wa mataifa katika miaka ya ya 2022, 2024 na 2026, kujadili ahadi za fedha za mazingira pamoja nakutoa malengo yakupunguza uzalishaji wa hewa chafu. Kiongozi wa chama cha Greens Adam Bandt amesema, hatua hii itafanya Australia iwajibike zaidi.

Wanajeshi wawili wa Jeshi la Ulinzi la Uganda (UPDF) wanaohudumu kwenye tume ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) wamehukumiwa kifo na wengine watatu wamehukumiwa kifungo cha miaka 39 jela kutokana na vifo vya raia. Mahakama ya Kijeshi ya Uganda iliendesha kesi mjini Mogadishu na imewakuta maafisa wawili hao na makosa ya kuua raia kwa makusudi karibu na ujirani wa Golweyne ilioko sehemu ya mkoa wa Lower Shabelle nchini Somalia Agosti mwaka 2021, na wengine watatu walihukumiwa kifungo cha jela kwa kushiriki katika uhalifu huo,” Waziri wa Sheria wa Somalia, Abdulkadir Mohamed Nur, ameiambia VOA Idhaa ya kisomali Jumamosi. Hukumu hii itakuwa fundisho kwa tume ya AMISOM kwamba hakuna atakaye weza kukimbia iwapo ataua raia wa Somalia,” Nur amesema.

Maafisa wa usalama wa Sudan wamefyatua gesi ya kutoa machozi dhidi ya maelfu ya waandamanaji katika sehemu mbali mbali za nchi hiyo, siku mbili baada ya jeshi kujaribu kuimarisha utawala wake kwa kuunda baraza jipya la utawala. Maandamano hayo ya kuunga mkono demokrasia yanafanyika karibu wiki tatu baada ya Jenerali Abdel Fatah al-Burhan kuipindua serikali, kuwafunga baadhi ya viongozi wa kiraia na kutangaza hali ya dharura nchini. Licha ya kufungwa kwa mawasiliano yote ya mtandao, mamia ya watu walikusanyika katika mji wa Ondurman karibu na mji mkuu wa Khartoum ambako polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji.


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Taarifa ya Habari 14 Novemba 2021 | SBS Swahili