Takwimu mpya zamakaazi zina onesha soko la nyumba zakupanga nchini Australia lina endelea kuwa baya, wakati uhaba wa nyumba zaku panga unasambaa hata katika sehemu za kandani na bei za nyumba zakupanga zikiendelea kuongezeka kuliko ukuaji wa mshahara.
Utafiti mpya umepata kuwa vijana chini Australia, wanataka haki yakuwa katika mazingira ya afya nzuri iwekwe ndani ya sheria, kuambatana na viwango vilivyo wekwa ng'ambo. Utafiti huo kutoka shirika la Australian Conservation Foundation, ume pata kuwa watu 9 kati ya 10 wenye miaka kati ya 13 hadi 24 nchini Australia, wanata Australia ifuate mfano wa zaidi ya nchi 160 duniani ambazo zime fanya geuzi hilo katika sheria zao.
Somalia imesema Jumapili kwamba mafuriko kutokana na mvua kubwa zinazonyesha yameua takriban watu 31 kwenye maeneo tofauti ya nchi. Karibu watu nusu milioni wamelazimika kuhama makwao kutokana na mafuriko nchini humo, huku maisha ya wengine milioni 1.2 yakiathiriwa, waziri wa Habari Daud Aweis amesema wakati akizungumza na wanahabari mjini Mogadishu.
Rais wa Kenya William Ruto Jumatatu wakati wa ufunguzi wa kikao kinachofanyika mjini Nairobi amesema kwamba wadau wa mkataba wa kwanza wa kimataifa wa kuzuia uchafuzi wa plastiki, wanahitaji kuharakisha mchakato huo.
Uganda inalilaumu kundi la ADF ambalo lina uhusiano na kundi la Islamic State kwa mauaji ya watalii waliokuwa kwenye fungate, wakiwa na muongozaji wao katika eneo pamoja na shambulio la shule lililosababisha vifo vya watu 42, wengi wao wakiwa wanafunzi. Waendesha mashtaka nchini Uganda wamemfungulia mashtaka kamanda wa kundi la wanamgambo wanaohofiwa kwa ugaidi na mauaji ya watalii wawili wa kigeni pamoja na dereva wao mwezi uliopita.