Mfumuko wa bei pamoja na kielezo cha bei ya mshahara viliongezeka kwa 0.8 ya asilimia katika wakati huo, nakufanya iwe mara ya kwanza katika muda wa miaka mitatu ambapo mishahara halisi haija rejea nyuma. Alipo zungumzia hoja hiyo mweka hazina wa taifa Jim Chalmers amesema Australia, inashuhudia ongezeko za mishahara ambayo Labor ili ahidi kabla ya uchaguzi mkuu uliuopita.
Mwanaume aliye lazimisha ndege ya Malaysia kurejea Sydney, baada yakutoa vitisho vya bomu, imeripotiwa kuwa ana matatizo mengi ya afya ya akili na anakataa kuondoka gerezani ili apelekwe mahakamani.
Jimboni Victoria zaidi ya jamuiya 80 zenye tamaduni na dini mbali mbali, zimejumuika katika bunge la jimbo hilo kuonga mkono Sauti yawa Australia wa kwanza Bungeni. Kundi hilo limesema lina kiri umuhimu wa nafasi ya utofauti wa jumuiya yazo, kufanikisha kutambuliwa katika katiba kwa wa Australia wa kwanza. Mkurugenzi mtendani wa shirika la Ethnic Communities’ Council of Victoria Mo Elrafihi amesema, jumuiya za tamaduni mbali mbali zina nafasi mhimu katika kura ya maoni ijayo.
Aliyekuwa rais wa Marekani Donald Trump na washirika wake 18, wamepatikana na mashtaka ya kujibu katika jaribio lao la kutaka kubatilisha matokeo ya uchaguzi mkuu mwaka 2020, katika jimbo la Georgia. Trump na washirika wake wanashutumiwa kwa kujaribu kuvuruga matokeo ya uchaguzi katika jimbo la Georgia ambalo alishindwa na rais Joe Biden. Anadaiwa kumshurutisha msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo, mrepublican, kutafuta kura za kutosha kumpa ushindi ili aendelee kusalia madarakani. Mashtaka hayo yanaelezea namna Trump alijaribu kuvuruga mashine za kupiga kura katika jimbo la Georgia.
Afisi ya Kamishna wa Kulinda Data imeelekea kortini kuomba amri kwamba data iliyokusanywa na kampuni ya Worldcoin ilindwe. Huku ikitaka kesi hiyo ishughulikiwe kwa dharura, afisi hiyo inataka Mahakama Kuu iamuru kwamba data zilizokusanywa kutoka kwa Wakenya ihifadhiwe vizuri, kusubiri kukamilishwa kwa uchunguzi unaendelea kubaini uhalali wa shughuli hiyo.
Shirika la kutetea haki za binadamu, Amnesty International imeitaka Mamlaka ya Tanzania kuwaachilia mara moja na bila masharti Willibrod Slaa, aliyekuwa mbunge na Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Boniface Mwabukusi, mwanasheria na mwanaharakati, na Mdude Nyagali, mwanaharakati wa kisiasa, ambao wote walikamatwa kati ya 12 na 13 Agosti kwa kosa la kukosoa suala la bandari. makubaliano kati ya Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Amnesty International imesema.