Muswada sasa umepita ndani ya nyumba ya wawakilishi, hatua ambayo sasa inaruhusu Marekani kuuza manowari yanayo tumia nishati ya nyuklia kwa nchi yoyote. Muswada huo, sasa utawasilishwa kwa Rais Biden, utiwe saini nakuwa sheria.
Wazima moto wame waokoa watu 18 katika mji mmoja wa Kaskazini Queensland, baada ya Kimbunga Jasper kufika katika eneo hilo usiku wa Jumatano Disemba 13 2023. Makumi yama elfu ya nyumba na biashara, yame achwa bila umeme na mvua nzito pamoja na upepo wa uharibifu.
Ma milioni yawa Australia wanapunguza matumizi yao na wengi wao hawana uwezo wakufanya matumizi ya ziada kwa sherehe za krismasi. Zaidi ya idadi yawa Australia milioni 5.3 hawata kuwa na uwezo wakumudu chakula cha krismasi mwaka huu na, 30% ya wazazi wana wasiwasi watoto wao hawata pata zawadi, utafiti wa shirika la Jeshi la Wokovu umepata. Utafiti huo umepata kuwa zaidi ya watu elfu 2000 wamepata kuwa takriban 60% walihisi mkazo zaidi katika msimu huu wa likizo kulinganisha na 31.6 katika wakati kama huo mwaka jana.
Shirika la Kimataifa la Fedha Duniani na Benki ya Dunia wameidhinisha msamaha wa deni la dola bilioni 4.5 kwa Somalia siku ya Jumatano. Baada ya nchi hiyo ya Pembe ya Afrika kukamilisha mageuzi miaka kadhaa ya kifedha chini ya mpango wa kuzipunguzia madeni nchi maskini maarufu kama Heavily Indebted Poor Countries Initiatives au HIPC. Mpango huo ulianzishwa na IMF na Benki ya Dunia mwaka 1996 ili kuzisaidia nchi maskini kuhimili madeni.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania siku ya Alhamisi imethibitisha kifo cha mmoja wa Watanzania ambaye “aliuawa mara baada ya kukamatwa na Hamas” wakati wa mashambulizi ya Oktoba 7, huko Kusini mwa Israel. Siku ya Alhamisi Waziri wa Mambo ya Nje, Januari Makamba amesema mamlaka “imearifiwa na serikali ya Israel kuwa Joshua Mollel, mwanafunzi wa Kitanzania aliyekuwa akisoma nchini Israel, ambaye alipoteza mawasiliano tangu Oktoba 7, 2023…aliuawa mara baada ya kukamatwa na Hamas.” Serikali ya Israel iliwataja wanafunzi wawili kutoka Tanzania waliokuwa wakisoma nchini Isreal -- Clemence Felix Mtenga mwenye umri wa miaka 22 na Joshua Loitu Mollel mwenye umri wa miaka 21.
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo inajiandaa na uchaguzi mkuu wa Desemba 20, lakini vijana wengi wanasema suala la msingi kwao ni amani na ajira, kwa ajili ya mustakabali wa taifa lao. Wapiga kura wanatarajiwa kupiga kura mnamo Desemba 20 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Rais Felix Tshisekedi, 60, anawania muhula wa pili. Vijana, ambao wengi wao wanakabiliwa na ukosefu sugu wa ajira -- wanaunda kundi muhimu la wapiga kura. Zaidi ya asilimia 60 ya wakaazi wa taifa hilo lenye watu milioni 100 wana umri wa chini ya miaka 20.