Taarifa ya Habari 15 Machi 2022

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS Swahili

Australia na Uholanzi zime zindua hatua zakisheria dhidi ya Urusi kwa kuangusha ndege ya M-H-17 ya Malaysia katika mwaka wa 2014.


Upinzani wa shirikisho umesema serikali haifanyi vyakutosha kupunguza gharama ya shinikizo ya maisha, wakati uvumi unaendelea kama serikali ita kata kodi ya mafuta. Hata hivyo Waziri Mkuu Scott Morrison amesema uamuzi wa serikali ya shirikisho kwa kodi ya mafuta, hauta tangazwa hadi bajeti ya taifa itakapo tangazwa 29 Machi 2022.

Ujumbe wa Ukraine na Russia umeanza tena mazungumzo ya amani Jumatatu, siku moja baada ya Rashia kufanya shambulio baya la kombora kwenye kambi ya kijeshi magharibi mwa Ukraine, kilomita 25 tu kutoka Poland, mwanachama wa NATO. Watu 35 waliuawa na wengine 134 kujeruhiwa katika shambulio hilo kwenye kituo cha kimataifa kwa ajili ya kulinda amani na usalama.

Kiongozi wa eneo lenye mamlaka ya kiasi, Somaliland, Muse Bihi Abdi ameitaka jumuiya ya kimataifa kulitambua eneo lake kama taifa huru, akisema mazungumzo na Somalia yameshindwa kuzaa matunda. Kiongozi huyo amesema katika mazungumzo yaliodumu kwa muongo mmoja, Somalia imeonesha hali ya kutokuwa na hamasa ya majadiliano yenye tija, na hivyo kuilazmisha Somaliland kuoimba utambuzi wa kimataifa wa kuwa taifa huru.


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Taarifa ya Habari 15 Machi 2022 | SBS Swahili