Wakati huo huo upinzani wa shirikisho umesema sera ya serikali ya Morrison kwa nyumba, utafanya nyumba ziwe ghali zaidi. Msemaji wa chama cha Labor kwa maswala ya makaazi na ukosefu wamakaazi Jason Clare, amesema mengi yanastahili fanywa kushughulikia swala la makaazi yakijamii na makazi ya gharama nafuu.
Mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu wa Kenya, Dkt William Samoei Ruto, amemtangaza mgombea wake mwenza kuwa ni Rigathi Gachagua. Bw Gachagua alikuwa anawania wadhifa huo dhidi ya Profesa Kithure Kindiki, wawili hao wataongoza mrengo wa Kenya Kwanza katika uchaguzi mkuu dhidi ya mrengo wa Azimio One Kenya unao ongozwa na Raila Odinga anaye tarajiwa kumtangaza mgombea mwenza Jumatatu 16 Mei 2022.
Serikali ya Tanzania imetangaza kupandisha kima cha chini cha mshahara wa wafanyakazi wa umma nchini humo kwa 23.3%. Rais wa taifa hilo la Afrika Mashariki, Samia Suluhu Hassan amesema ameridhia mapendekezo ya nyongeza ya mshahara yaliyo wasilishwa Ikulu, ikiwa ni muendelezo wa kikao cha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye alipokea taarifa ya watalaamu mjini Dodoma kuhusu suala la nyongeza ya mshahara.