Wanajeshi katika jimbo la kaskazini mwa Ethiopia la Tigray wamefyatua maroketi katika jimbo jirani, katika mzozo wao na serikali ya Ethiopia unaoendelea kupanuka.
Tume ya uchaguzi nchini Uganda imepiga marufuku mikusanyiko ya watu wakati wa kampeni kuelekea uchaguzi mkuu mwaka ujao 2021. Marufuku hiyo imetolewa siku moja baada ya rais Yoweri Museveni kusema kwamba wagombea wenzake wanakusanya watu licha ya kuwepo janga la virusi vya Corona, watachukuliwa hatua haki.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema serikali itakuwa na jukumu kuu kuanzia mikakati ya kuwakinga raia wake dhidi ya janga la virusi vya corona, kuwekeza kwa vijana na kutatua tatizo sugu la umiliki wa ardhi.