Watetezi wa haki za binadamu, wamiliki wa vyombo vya habari, waandishi wa habari na viongozi mbalimbali wamekosoa agizo la tume ya mawasiliano nchini humo kutaka mitando yote ya kijamii inayotumika kusambaza habari na maudhui kusajiliwa.
Wanafunzi 10 wamepoteza maisha na wengine saba kujeruhiwa vibaya baada ya shule ya msingi Byamungu Islamic Mkoani Kagera kuungua kwa moto usiku wa kuamkia Jumatatu. Taarifa za awali zinaeleza kuwa umri wa wanafunzi waliofariki katika shule hiyo iliyoko kata ya Itera wilayani Kyerwa ni kati ya miaka sita hadi 12.
Kwa mara ya kwanza tangu kukamatwa kwake mmoja wa wapinzani wakuu wa serikali ya Rwanda Paul Rusesabagina amefikishwa kizimbani mjini Kigali nchini Rwanda akikabiliwa na mashitaka ya ugaidi. Paul Rusesabagina alipata umaarufu mkubwa kupitia filamu maarufu kama Hotel Rwanda. Anashutumiwa kuendesha mauaji ya raia wasio na hatia kupitia mashambulizi ya kundi la wapiganaji wa FLN kusini magharibi mwa Rwanda miaka miwili iliyopita.