Utafiti mpya umeonesha kuwa wakimbizi wanakabiliana na maswala yanayo endelea yakutengwa na familia zao pamoja na ujumuishi kidijitali. Ripoti mpya kutoka shirika la Settlement Services International na chuo cha Western Sydney imesema kuwa, wakati wakimbizi wapya nchini wanahisi wako sehemu ya Australia, bado wanakabiliana na na ongezeko la dhiki yakisaikolojia kupitia muda mrefu wakutengwa na familia.
Risala za pongezi zimetolewa kwa rais mteule wa Kenya William Ruto ambaye ametangazwa mshindi wa kinyan'anyiro kilichokuwa na ushindani mkali. Mwenyekiti wa IEBC alitangaza kuwa Dr Ruto alipata kura milioni 7,176, 141 ambayo ni asili mia 50.49 ya kura zote zilizopigwa dhidi ya mpinzani wake wa karibu, mwanasiasa mkongwe, Raila Odinga aliyepata kura milioni 6,942,930, sawa na asili mia 48.85 ya kura zote.
Wizara ya afya ya Zimbabwe imesema Jumapili kwamba mlipuko wa Surua umeua watoto 80 nchini humo tangu Aprili, wakati ikidai mikusanyiko ya kidini imesababisha kuongezeka kwa maambukizi. Jimbo la Manicaland mashariki mwa Zimbabwe linasemekana kuongoza kwa maambukizi. Chimedza ameongeza kusema kwamba kesi ya kwanza iliripotiwa Aprili 10 na tangu wakati huo maambukizi yameenea kote nchini, yakisemekena kuchochewa zaidi na mikusanyiko ya waumini makanisani.