Mamia yamaelfu yawa australia itabidi wasafiri nje ya maeneo bunge yao, kupata zahanati ya GP inayo toa huduma ya bulk billing kwa wagonjwa wapya. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa na saraka ya huduma ya afya Cleanbill, ambayo ilipata kuwa ni 35% tu ya zahanati za GPs nchini Australia ambazo hutoa chaguzi la builk billing, kwa wagonjwa wapya ambako madaktari hutuma bili kwa Medicare badala yawagonjwa.
Kiongozi wa Magharibi Australia Mark McGowan, ame elezea shambulizi dhidi ya walinzi katika kitengo cha vijana ndani ya gereza la Casuarina usiku wakuamkia kuwa inasikitisha nakushangaza. Mlinzi wa kike alishambuliwa na mfungwa kwa chuma, wakati wa mazoezi mchana wa jumamosi.
Kikosi Maalum cha Wanamgambo nchini Sudan cha RSF, kimesema kimechukua udhibiti kamili wa Ikulu ya rais, makaazi ya mkuu wa jeshi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Khartoum. Katika taarifa yake iliyotolewa Jumamosi, RSF imesema imechukua pia udhibiti wa viwanja vingine viwili vya ndege, kwenye mji wa kaskazini wa Merowe na mji wa El-Obeid ulioko upande wa kusini mwa nchi.
Waziri wa fedha Uganda amekamatwa kwa madai ya kuiba mabati, mabati hayo yalitengwa kwa ajili ya makazi ya gharama nafuu huko Karamoja eneo ambalo halina maendeleo na halifuatiliwi huko kaskazini magharibi mwa Uganda linapakana na Kenya na Sudan Kusini.
Polisi nchini Kenya walisema Ijumaa kuwa wameanzisha msako wa kumtafuta kiongozi wa dhehebu la kidini nchini humo kufuatia vifo vya waumini wanne ambao inasemekana aliwaambia wasile ili "kukutana na Yesu".