Polisi jimboni New South Wales wamefungua mashtaka kwa takriban idadi ya watu 600, kwa makosa makubwa ya unyanyasaji wa nyumbani, katika oparesheni maalum jimboni kote. Oparesheni hiyo ya siku nne ime zalisha mashtaka 1107 ya unyanyasaji wa nyumbani kufunguliwa dhidi ya watu 592, pamoja na mihidarati, bunduki na na silaha zingine kuchukuliwa.
Serikali ya Victoria imetangaza mageuzi mapya ya kamari kupunguza, madhara ndani ya sehemu ambako kuna mashine zaki elektroniki za kamari kote jimboni. Takriban watu wa Victoria laki tatu elfu 30 wamepitia uzoefu wa madhara kwa sababu ya kamari kila mwaka, hali ambayo inagharimu jimbo hilo $7 bilioni kila mwaka.
Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya uhalifu ya kimataifa ICC Karim Khan, amesema kwamba ofisi yake inchunguza ripoti kwamba miili ya watu 87 ilipatikana katika kaburi la pamoja katika jimbo la Dafur, maghaaribi mwa Sudan.
Waziri wa ujenzi na uchukuzi wa Tanzania Profesa Makame Mbarawa ametetea hatua ya serikali kuingia makubaliano ya ushirkiano na kampuni ya DP World akitaja uwezo mkubwa wa kampuni hiyo kuwezesha bandari kote duniani. Hii na mara ya kwanza kwa serikali kujitokeza kwa wahariri wakati sakata la mkataba huo likiendelea kuwa mada moto inayojadiliwa kila uchao.
Chama cha upinzani cha Ensemble pour la République kinachoongozwa na Moise Katumbi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kimetaka ufanyike uchunguzi huru baada ya kuuawa mbunge wake, Chérubin Okende siku ya Alhamisi. Mwili wake uliojaa matundu ya risasi ulikutwa Alhamisi asubuhi katika gari lake kwenye mmoja barabara za mji mkuu, aliongeza afisa huyo.