Jeshi la Korea Kaskazini limeonya kwamba liko tayari kuingia katika eneo lisiloruhusiwa shughuli za kijeshi linalogawanya nchi hiyo na Korea Kusini.
Baada ya kifo cha rais wa Burundi hayati Pierre Nkurunziza mapema wiki hii, Mahakama ya Katiba imechukua imeagiza kutawazwa kwa rais mteuli Jenerali Evariste Ndayishimiye.
Wafanyakazi wanne wa Ikulu ya rais nchini Kenya wamepatikana na virus vya corona. Kwa mujibu wa msemaji wa Ikulu Kanze Dena, wafanyakazi hao waligunduliwa wameambukizwa COVID-19 baada ya kufanyiwa uchunguzi Alhamisi, Juni 11.