Serikali ya shirikisho inatetea uwekezaji wake kwa jibu la huduma ya uzeeni, kwa matokeo ya uchunguzi wa tume yakifalme katika sekta ya huduma ya uzeeni. Serikali itawekeza bilioni 17.7 za dola katika muda wa miaka minne ila, wanaharakati wa huduma ya uzeeni pamoja na upinzani wamesema uwekezaji huo bado haujatosha.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ameelezea kusikitishwa kwake na mashambulio ya anga ya jeshi la Israel yaliyolenga na kuliharibu jengo la ghorofa 12 kwenye Ukanda wa Gaza. Jengo hilo lilikuwa na ofisi kadhaa za mashirika ya habari ya kimataifa na pia makazi ya watu.
Mahakama Kuu ya Kenya, Alhamisi usiku iliamuru kwamba mchakato uliokuwa ukiendelea wenye nia ya kuifanyia marekebisho katiba ya nchi hiyo ya mwaka wa 2010, si halali. Majaji watano waliokuwa wakisikiliza hoja tisa za kupinga kwendelea kwa mchakato huo, walikubaliana kwa kauli moja kwamba kamati ya BBI iliyoundwa na Rais Uhuru Kenyatta na aliyekuwa hasimu wake wa kisiasa Raila Odinga ilikiuka sheria na katiba ya nchi hiyo.