Kiongozi wa upinzani Peter Dutton amesema pendekezo laku ongeza masaa ya kazi kwa wanao pokea malipo ya JobSeeker, itawaruhusu walipwe zaidi wakati inapunguza shinikizo kwa bajeti. Chama cha mseto kimeomba nyongeza ya kati ya masaa 5 hadi 10, kwa masaa ambayo watu wanao lipwa JobSeeker wanaweza fanya kazi kabla malipo yao ya athiriwe.
Biashara mbili za vyakula jimboni Victoria, zina kabiliwa kwa mamia yamashtaka kwa tuhumza zakuvunja sheria zakuajiri watoto. Red Rooster ambayo iko Wodonga imefunguliwa mashtaka ya uhalifu 355, wakati kampuni ya Cold Rock inayo uza ice cream Shepparton, inakabiliwa kwa mashtaka ya uhalifu 124.
Kenya na Somalia Jumatatu zimekubaliana kufungua tena vituo vitatu vya mpaka kati ya nchi hizo mbili baada ya kufungwa kwa miaka 12 kutokana na ukosefu wa usalama na vitisho vinavyohusiana na ugaidi.
Baadhi ya maduka katika eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania huenda yakaendelea kufungwa kufuatia mgomo wa wafanyabiashara wanaopinga rushwa na malimbikizo ya kodi wanayotozwa na Mamlaka ya Mapato nchini Tanzania (TRA).