Mamia ya watu katika mji wa kati magharibi jimboni NSW wa Forbes, wame amriwa kuondoka mjini humo kabla ya mafuriko makubwa ambayo yametabiriwa. Amri hiyo yakuondoka ilitolewa na huduma ya dharura ya jimbo [[SES]] mida ya saa tano asubuhi ya leo jumanne 16 Nov. Onyo hilo linawahusu wakaaji takriban elfu mbili waondoke kabla ya saa tatu unusu usiku wa leo. Takriban nyumba 800 zinatarajiwa kufurikwa, na mto Lachlan unatarajiwa kufikisha au kupitiza viwango vya hatari vya mafuriko vilivyo rekodiwa katika mwaka wa 2016.
Rais wa Marekani Joe Biden amezungumza kwa njia ya vidio na mwenzake wa China Xi Jinping, katika mkutano ambao viongozi wote wawili wamesema unalenga kupunguza mivutano isiyo ya lazima baina ya madola hayo yenye nguvu. Mkutano huo uliosubiriwa kwa hamu ulifunguliwa kwa viongozi hao wawili kupungiana mkono baada ya kuonana kupitia televisheni katika kile mtu angeweza kukifananiasha na mikutano mingine kwa njia ya video ambayo imekuwa ya kawaida tangu kuzuka kwa janga la Corona.
Shambulizi la wanamgambo dhidi ya kituo cha polisi kaskazini mwa Burkina Faso limeua maafisa 19 na raia mmoja. Wizara ya usalama imesema kwamba shambulizi limetokea katika mji wa Inata, mkoa wa Soum, karibu na mpaka wa Burkina Faso na Mali. Waziri wa usalama Maxime Kone, amesema huenda idadi ya waliokufa ikaongezeka.