Waziri Mkuu wazamani Julia Gillard ataongoza tume yakifalme kwa elimu ya mapema katika jimbo la Kusini Australia, tume hilo litachunguza jinsi jimbo hilo linaweza leta mbele umri wakuanza masomo kutoka miaka 4 hadi miaka 3. Serikali ya chama cha Labor ime ahidi kuwapa watoto wenye miaka 3 fursa yakuanza masomo ya chekechea kuanzia 2026.
Chama cha The Greens kimeomba malipo yote ya msaada yaongezwe kwa angalau $88 kwa siku kujaribu kupunguza umasikini nchini Australia. Chama hicho kimesema zaidi yawa Australia milioni 3 wanaishi katika umasikini, mtoto mmoja kati watoto 6 wakijumuishwa katika takwimu hiyo.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza amri ya kutotoka nje ya wiki tatu kwa wilaya mbili zilizoathirika kuzuia maambuzi ya ugonjwa wa Ebola ya Sudani. Amri hiyo ni sehemu ya masharti 21 ya kukabiliana na mlipuko mpya wa ugonjwa huo uliotangazwa nchini humo Septemba 20, 2022. Mpaka kufikia jana watu 58 wamethibitishwa kuambukizwa Ebola, 19 wamefariki na 20 wamepona wakiwemo Madaktari na wafanyakazi wa sekta ya afya.