Waziri wa maswala yakigeni Penny Wong amesema kundi hilo lime ondoka kwa ndege kutoka mjini Tel Aviv, nakuwasili mjini Dubai ndani ya ndege iliyo kodiwa pamoja na ndege mbili za jeshi la Australia. Seneta Wong amesema safari za uhamisho kutoka Gaza, pamoja na safari zakurejesha raia nyumbani, zinategemea hali ya usalama inayo badilika kwa kasi.
Serikali ya Tanzania imesema imeandaa mpango wa kuwarejesha nyumbani raia wake walio nchini Israeli wakati mzozo ukiendelea kati yake na wanamgambo wa Hamas. Taarifa iliyotolewa na wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania Jumamosi ilitoa wito kwa “Watanzania walio tayari kurejea nyumbani kujiandikisha kwenye Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uliopo Tel Aviv.
Kuna uwezekano wa Australia hawatapata fursa ya pili, kuwatambua wa Australia wa kwanza ndani ya katiba ya nchi katika siku za usoni, licha ya ahadi ya chama cha upinzani. Kura ya maoni ya Sauti yawa Australia wa kwanza ilifeli katika uchaguzi wa jumamosi, wakati majimbo yote yalipinga pendekezo hilo, ila wilaya ya ACT tu ndiyo iliyo piga ya ‘Ndio’ kwa wingi. Katika siku za kabla ya uchaguzi huo, kiongozi wa upinzani Peter Dutton, ali ahidi upinzani wa mseto uki unda serikali, uta itisha kura ya pili ya maoni itakayo fanya geuzi rahisi lakuwatambua wa Aboriginal na wanavisiwa wa Torres Strait ndani ya katiba.
Ila alipo ulizwa jumatatu 16 Oktoba, kama bado ana nia yaku itisha kura ya pili ya maoni akichuguliwa kuongoza Australia, Bw Dutton alikwepa swali hilo.
Wakati huo huo waziri wa Mazingira Tanya Plibersek, amesema serikali ya shirikisho itachunguza sababu za kufeli kwa kampeni ya Ndio yakuwatambua wa Australia wa kwanza bungeni, kwa ajili yaku amua hatua zitakazo fuata kuendelea mbele. Takriban wapiga kura 60% wali piga kura ya La.
Mvua kubwa iliyonyesha kusini mwa Burundi imesababisha vifo vya watoto wanne baada ya kanisa walimokuwa kuporomoka huku watu wengine 15 wakijeruhiwa siku ya Jumapili, kulingana na afisa wa eneo hilo na vyombo vya habari vya serikali. Mvua kubwa ikiandamana na upepo mkali ilianza kunyesha Kiyange mwendo wa saa moja asubuhi, afisa wa serikali ya mtaa Esperance Inarukundo aliliambia shirika la habari la AFP.
Jeshi la Afrika Kusini lilisema Jumapili kuwa limewaamuru kurudi nyumbani wanajeshi wanane wanaotuhumiwa kwa utovu wa nidhamu unaohusiana na unyanyasaji wa kingono katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hadi uchunguzi ufanyike. Wanane hao, sehemu ya ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa (Monusco), walizuiliwa kwenye kambi zao katika mji wa mashariki wa Beni mapema mwezi huu.
Katika michezo,
Wanachama kadhaa wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki walitoa wito Jumapili kwa Rais Thomas Bach kusalia katika wadhifa huo baada ya muhula wake wa pili kumalizika mwaka 2025 na kuendelea kwa muhula wa tatu, hali ambayo haijawahi kushuhudiwa.
Bach alichaguliwa mwaka wa 2013, na anatarajiwa kuachia nafasi hiyo mwaka 2025 kwa mujibu wa kanuni za sasa za Olimpiki, kufuatia muhula wa kwanza wa miaka minane na wa pili wa miaka minne. IOC, hata hivyo, ilisema itajadili suala hilo katika mkutano ujao wa bodi kuu.
Katika soka Manchester City ina amini sasa wanaweza muona Mary Fowler halisi, baada ya nyota huyo wa timu ya wanawake ya taifa almaarufu Matildas, kupongezwa kwa kusaidia timu yake kupata ushindi wa magoli tano kwa sufuri dhidi ya Bristol City, hali ambayo ime iweka timu hiyo ya Sky Blues katika kilele cha ligi kuu ya wanawake nchini England inayo julikana kwa jina la Women's Super League (WSL). Fowler hakuwa akitajwa sana katika msimu wake wa kwanza, ila mchezaji huyo mwenye miaka 20 kwa mara nyingine ameonesha kipaji chake jumapili, kuwa sasa yuko tayari kuonesha uwezo wake katika WSL baada ya alivyo onesha katika kombe la dunia la wanawake.
Wakati huo huo Sam Kerr, naye amenguruma katika orodha ya wafungaji, baada yaku saidia timu ya wanawake ya Chelsea kuishinda West Ham kwa magoli 2-0.