Chama cha upinzani nchini cha toa onyo kuwa mfumo wa Medicare uko hatarini, baada ya uteuzi wa atakaye kuwa waziri wa afya, serikali ya mseto ikishinda uchaguzi mkuu hata hivyo serikali ya mseto imekanusha tuhuma hizo.
Mivutano ya zaidi ya mwaka mmoja imemalizika baada ya wabunge wapya wa baraza kuu la bunge la Somalia kukutana kwa mara ya kwanza Jumamosi kuanza utaratibu wa kumchagua rais. Bunge jipya la Somalia limekutana kwa mara ya kwanza Jumamosi katika kile kinachoelezewa ni hatua muhimu kuelekea kukamilisha mchakato wa kumteua rais mpya. Wasomali huwa hawapigi kura moja kwa moja kuwachagua wawakilishi wao au rais katika taifa hilo linalokumbwa na vita.
Ndege za kivita za Russia zimeshambulia kwa mabomu mji wa Lviv na kwa makombora mji mkuu wa Kyiv Jumamosi, na kusababisha kifo cha mtu mmoja baada ya karibu wiki mbili za utulivu katika mji mkuu wa Ukraine. Kuongezeka kwa mashambulizi kunatokea siku moja baada ya Moscow kutoa tena vitisho vya kushambulia kwa makombora ya masafa marefu miji mbalimbali ya Ukraine baada ya manwari yake kuu ya kivita Moskova kuzama katika bahari ya Black Sea.