Majimbo yote 50 ya Marekani yamewekwa katika hali ya tahadhari kutokana na uwezekano wa maandamno ya ghasia wikendi hii , kabla ya kuapishwa kwa rais mteule Joe Biden siku ya Jumatano. Vikosi vya ulinzi wa kitaifa vimetumwa kwa wingi katika mji wa Wshington DC ili kuzuia kuzuka kwa ghasia mbaya za wiki iliopita.
Tume ya Uchaguzi nchini Uganda, ilitangaza Jumamosi kwamba Rais Yoweri Museveni ameshinda kura ya urais baada ya kupata kura 5,851,037 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine, aliyezoa kura 3,475,298. Kyagulanyi amepinga matokeo hayo.
Afrika Kusini Ijumaa imechelewesha kuanza kwa mwaka mpya wa masomo kwa kipindi cha wiki 2 hadi Februari 15, ili kuzizuia shule zisiwe vituo vya maambukizi ya covid 19. Wakati huohuo kumeripotiwa kesi mpya za maambukizi 20,000 kwa siku wiki iliyopita.