Serikali ya Victoria imetangaza mfuko wa uwekezaji wenye thamani ya dola milioni 162 leo jumapili, ambazo zitawekeza takriban nafasi za wataalam 400 wa ziada kaitka hospitali kubwa 12 katik amiji ya Melbourne na Geelong.
Serikali ya shirikisho imetetea uamuzi wake wakuchelewa kurejesha malipo ya likizo ya janga, baada yakusisitiza awali kuwa haitaweza rejesha uwekezaji huo. Mweka hazina wa taifa Jim Chalmers amesema ukosaji kutoka msemaji wa upinzani Sussan Ley [[Lee]] haufai, baada yakusema kuwa serikali ili lazimishwa kurejesha malipo hayo ya $750 kwa watu ambao hawakuwa na likizo ya wagonjwa ambayo wangetumia kufunika muda wakujitenga kwa sababu ya UVIKO.
Shirika la Amnesty International limemuandikia barua rais wa Tanzania Suluhu Samia Hassan, kutaka oparesheni maalum ya kuwafurusha watu wa jamii ya wamaasai kutoka Loliondo katika mbuga ya taifa ya Serengeti, kusitishwa mara moja. Katika barua hiyo, shirika la Amnesty International linamsihi rais Samia kutoa maagizo ya kuacha mara moja hatua ya kuwaondoa wamaasai kutoka sehemu hiyo hadi “wamaasai watakaporidhia bila kushurutishwa na waondoke kwa hiari yao baada ya mashauriano ya wazi na haki.” Shirika hilo vile vile linataka uchunguzi huru na wa kina ufanyike kuhusu makabiliano yaliyotokea kati ya maafisa wa usalama na wamaasai mwezi Juni tarehe 9.