Taarifa ya Habari 17 Julai 2023

City - Swahili.jpg

Watendaji wa kampuni ya ushauri ya Deloitte wafika mbele ya kikao cha Seneti baada ya kuvuja kwa sakala la ushuru la kampuni ya PwC.


Wanachama wa kampuni hiyo kubwa ya uhasibu, wali eleza kamati hiyo kuwa kulikuwa maswala mhimu 121 katika mwaka huu wa fedha, ambayo yalijumuisha kesi moja ya ulaghai na kesi moja yakutumia vibaya taarifa ya serikali.

Baraza la Biashara la Australia limeomba maboresho ya matokeo ya ajira kwa watu ambao wana ulemavu. Ripoti ya baraza hilo imepata kuwa 92% ya wanachama wake wanataka kuwaajiri watu wengi wenye ulemavu katika nguvu kazi yao.
Corine Strauss ni Mkurugenzi mtendaji wa shirika la Australian Network on Disability, amesema biashara nyingi mara nyingi huwa wazi kufanya sehemu zao za kazi kuwa jumuishi ila, hazi jui pakuanzia.

Waziri wa mazingira Tanya Plibersek amesema serikali ya Labor bado iko katika sehemu imara, licha ya matokeo ya kura ya maoni kuonesha uungwaji mkono wa chama cha Labor uko katika kiwango cha chini zaidi tangu uchaguzi wa 2022.

Mwaka 2023 hadi sasa haujawa mzuri kwa Afrika. Mgogoro uliozuka nchini Sudan, umezidi kuongezeka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kuenea kusini kutoka Sahel. Uchumi wa nchi nyingi za Afrika unakabiliwa na madeni makubwa. Lakini mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anapendelea kuzingatia ahadi ya bara hilo; hasa, jinsi ya kutumia vizuri mali zake kutokana na utajiri wake mkubwa wa maliasili hadi nguvu kazi yake kubwa, na ya vijana kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa, kuwekeza katika maendeleo endelevu na uchumi wa kijani kukua.

Kundi la waasi limeua watu 11 kaskazini mashariki mwa Congo, afisa wa eneo hilo amesema Jumapili. Isaac Kibira, naibu mkuu wa mtaa wa Bwito katika mkoa wa Kivu Kaskazini, amesema watu hao waliuawa na waasi wa M23. Miili ya raia 11 ilipatikana Jumapili asubuhi, iliachwa kwenye safu mbili kwenye nyasi.

Katika michezo,
Kuna wito kwa shirika la soka duniani FIFA, kutekeleza ahadi yake ya kuhakikisha usawa wa jinsia katika soka, kama kombe la dunia la wanawake la 2023 lita acha alama yakudumu kwa mchezo huo.

Dr Michelle O'Shea kutoka chuo cha magharibi Sydney amesema FIFA inastahili toa ahadi yake kwa maandishi, kwa ahadi iliyo toa mapema mwaka huu kuwa hela za zawadi ya mshindi zitakuwa sawa kufikia mwaka wa 2027.

Hela za ushindi za kombe la dunia la wanawake la 2023, zitakuwa robo ya hela iliyo tolewa kwa wanaume katika michuano ya mwaka jana.






Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Taarifa ya Habari 17 Julai 2023 | SBS Swahili