Joe Biden ametoa angalizo kuwa "watu wanaweza kufa" kama rais aliye madarakani ataendelea kuwa kuzuizi. Akizungumza mjini Delaware, rais mteule alisema ushirikiano aliokuwa anauhitaji ni kukabiliana na mlipuko wa janga la corona.
Viongozi wa nchi za Afrika wameanza Jumatatu juhudi za kutafuta suluhisho kwa mzozo unaozidi kuongezeka nchini Ethiopia, siku mbili baada ya roketi kushambulia mji mkuu wa Eritrea na kuzusha hofu kwamba ugomvi huwenda ukaenea. Rais Yoweri Museveni wa Uganda amekutana na naibu waziri mkuu, ambae pia ni waziri wa mambo ya nje wa Ethopia, Demeke Mekonnen hii leo mjini Gulu, Kaskazini mwa Uganda, kuzungumzia hali ya huko Tigray.
Shirika la kutete haki za kibinadamu nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ACAJ, linataka maafisa wa usalama nchini humo kumwachilia huru mwanamziki maarufu Tshala Muana ambaye alikamatwa jumatatu mjini Kinshasa. Polisi wamemkamata mwanamziku huyo mweye umri wa miaka 62 baada ya kutoa wimbo ambao wachambuzi nchini humo wanasema kwamba tafsiri yake inamdalilisha rais wa sasa Felix Tshisekedi, japo wimbo huo hautaji mtu yeyote.