Upinzani wa shirikisho waendelea kuikosoa serikali ya Labor, kwa kutochukua hatua thabiti zaku linda umma na waathiriwa wa wahalifu wanao achiwa huru baada ya hukumu ya mahakama ya upeo.
Waziri wa Afya atangaza uwekezaji mpya zaidi ya milioni mia moja zitakazo tumiwa kuwaajiri zaidi ya wauguzi 100 watakao wahudumia wagonjwa wenye saratani kote nchini.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatano lilitoa wito wa “kuongezwa muda wa kusitisha mapigano kwa ajili ya kibindamu” huko Ukanda wa Gaza. Baraza hilo likiachana na majuma kadhaa ya kutochukua hatua na mabishano, hasusani kwa ajili ya ulinzi wa watoto, lakini Israel haraka imekataa hatua hiyo.
Wabunge nchini Kenya Alhamisi wameidhinisha hatua ya kupeleka maafisa polisi 1000 nchini Haiti. Operesheni iliyoidhinishwa na Umoja wa Mataifa, kwa lengo la kulisaidia taifa hilo la Caribbean, kukabiliana na tatizo la ghasia za magenge. Mwezi Julai Kenya iliahidi kupeleka maafisa 1,000 wa polisi nchini humo, baada ya ombi la kimataifa la Haiti la maafisa wa usalama, ili kusaidia katika kukabiliana na magenge yanayolaumiwa kueneza uhalifu.