Taarifa ya Habari 17 Oktoba 2023

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Serikali ya shirikisho imesema inaendelea kufuatilia hali inayo endelea kudorora mjini Gaza, wakati Israel ina andaa kufanya mashambulizi ya nchi kavu baada ya hatua yakuzingira mji huo, ambayo mashirika ya msaada yamesema inachangia katika mgogoro wakibinadam.


Ndege mbili zilizo fadhiliwa na serikali ya Australia zime tua mjini Dubai, zikiwa na takriban abiria 200 wanao hamishwa kutoka Israel.

Wakimbizi wame jumuika katika bunge la taifa mjini Canberra kutoka sehemu zote za Australia wiki hii, kuomba viza zao za muda zibadilishwe kuwa zakudumu. Muunganiko wa wakimbizi mjini Canberra ume anza leo Oktoba 17, ambako vikundi vya wakimbizi takriban elfu 12 ambao wana viza za muda au bila kuwa na viza, wana jumuika nje ya bunge la taifa.

Vijiji vilivyochomwa pamoja na vijana waliovalia sare za kijeshi ni miongoni mwa yale yanayoshuhudiwa kati ya Goma mji wa mashariki mwa DRC na ule wa Kitshanga uliopo tajkiban umbali wa kilomita 80. Waasi wa M23 na wanamgambo watiifu kwa serikali ya Congo wamekuwa wakipambana kwenye eneo hilo katika siku za karibuni kinyume na makubaliano tete ya sitisho la mapigano ambalo lilidumu kwa miezi kadhaa. Katika ushindi nadra dhidi ya M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda, wanamgambo watiifu mwezi huu wameukomboa mji wa kimkakati wa Kitshanga kwenye jimbo la Masisi, Kivu Kaskazini.

Viongozi wa mataifa yanayoinukia kiuchumi wanakutana nchini China kwa kongamano ambalo litaadhimisha miaka 10 ya mradi wa kimataifa wa ujenzi wa miundombinu ya reli na barabara, huku Kenya ikisaka mikopo zaidi. Katika hatua nyingine, Rais William Ruto wa Kenya ambaye pia anahudhuria kongamano hilo anatafuta mkopo wa dola bilioni moja kutoka China, licha ya kuongezeka kwa deni la umma la nchi hiyo ambalo sasa limefikia dola bilioni 70. Hii ni kulingana na takwimu za hazina ya kitaifa ya mwaka 2022/2023.

Mamlaka nchini Eritrea ilisema "haitavutiwa" katika mazungumzo kuhusu ufikiaji wa Ethiopia kwenye Bahari Nyekundu kufuatia maoni yenye utata kutoka Addis Ababa.
Akiwahutubia wabunge, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alisema kuifikia Bahari Nyekundu ni "suala la kuwepo" kwa nchi yake. Ethiopia imekuwa nchi kubwa zaidi barani Afrika isiyo na bandari kufuatia Eritrea kujitenga nayo mwaka 1993. Tangu wakati huo imekuwa ikitegemea jirani yake mdogo Djibouti kwa zaidi ya 85% ya uagizaji na mauzo ya nje.



Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service