Mradi ambao unaweza saidia kuokoa maisha ya wahanga wa unyanyasaji wa nyumbani, unatarajiwa kupanuliwa kwa zaidi ya mahakama 134 za New South Wales. Serikali ilitangaza kuwa mradi huo wa jaribio wa mwaka mmoja, ambao ulikuwa unatarajiwa kuisha tarehe 31 Oktoba, sasa utaongezewa muda kwa mwaka mwingine mmoja kwa mahakama 61 kuanzia Novemba.
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitoa wito kwa pande zinazopigana nchini Sudan kusitisha mara moja uhasama huku mjumbe wake mjini Khartoum akisema takriban watu 200 wameuawa na mapigano hayo. Mapigano hayo yalizuka baada ya wiki kadhaa za myukano wa kuwania madaraka kati ya majenerali wawili walionyakua mamlaka katika mapinduzi ya mwaka 2021. Mkuu wa jeshi la Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, na makamu wake, Mohamed Hamdan Daglo, ambaye anaongoza Kikosi chenye nguvu cha Wanajeshi wa Msaada wa Haraka (RSF).
Idara ya taifa ya kuratibu dawa ya Nigeria Jumatatu imeidhinisha chanjo ya Malaria iliyotengezwa na chuo kikuu cha Oxford, ikiwa nchi ya pili kuchukua hatua hiyo baada ya Ghana iliyofanya hivyo wiki iliyopita. Ugonjwa wa Malaria unaosababishwa na mbu huuwa zaidi ya watu 600,000 kila mwaka, wengi wao wakiwa ni watoto wachang na wadogo barani Afrika. Nigeria ambayo ina idadi kubwa sana ya watu barani humo ndiyo iliyoathiriwa zaidi na Malaria, ikiwa na asilimia 27 za maambukizi na asilimia 32 ya vifo kutokana na Malaria ulimwenguni, kwa mujibu wa ripoti ya WHO ya 2021. Haijabainishwa ni lini chanjo hiyo itakapoanza kutumika Nigeria na Ghana, kwa kuwa WHO inaendelea kutathmini matumizi pamoja na usalama wake.