Jeshi la polisi la Victoria lasema lakaribia kuwakamata mashabiki walio shambulia uwanja nakumjeruhi mchezaji katika debi ya Melbourne.
Mkutano wa Viongozi wa Marekani na Afrika wamalizika pande zote zikiridhia malengo yaliyofikiwa, na Bunge la Msumbiji laidhinisha mswaada wa kuhalalisha wanamgambo kushiriki katika vita jimbo la Cabo Delgado
Nchini Uganda, Rais Museveni aondoa vizuizi vyote vya Ebola, akisema kuwa nchi hiyo ya Afrika Mashariki imepiga hatua katika kukabiliana na ugonjwa huo hatari. Museveni amefuta vizuizi vyote vilivyowekwa katika wilaya ya Mubende, ambayo ndio ilikuwa kitovu cha ugonjwa huo, kulikoshuhudiwa visa 66 vya maambukizi na vifo 29, na katika eneo la Kassanda lililokuwa na visa 49 na vifo 21.
Viwanjanni mbichi na mbivu kubainika katika fainali ya kombe la dunia kati ya France na Argentina, Croatia yaibuka mshinid wa mechi yakuwania mshindi wa tatu dhidi ya Morocco.