Taarifa ya Habari 18 Disemba 2023

City - Swahili.jpg

Baadhi ya wakaaji katika eneo la Kaskazini Queensland wamelazimika kupanda juu ya paa za nyumba zao, wakisubiri kuokolewa, wakati mvua nzito iliyo sababishwa na kimbunga chaki tropiki Jasper inasababisha mafuriko katika kanda hiyo.


Mtoto ni miungoni mwa kundi la watu walio kwama juu ya paa ya Hospitali moja ya kijijini katika sehemu nyingine ya jimbo hilo, kuliko athiriwa kwa kimbunga hicho.
Vyombo vya kufanya shughuli yakuokoa, vimetumwa na jeshi la wanamaji nalo lime itwa kutoa msaada wakati utabiri wa mvua, unaendelea kutabiriwa kwa siku ya Jumatatu hadi Jumanne. Baadhi ya sehemu za Kaskazini Queensland zimegongwa kwa zaidi ya mita moja ya maji na viwango hivyo vinatarajiwa kuvunja rekodi ya mwaka 1977, wakati mafuriko katika mji wa Cairns, tayari yako katika viwango vya rekodi. Mji huo tayari haufikiki kwa sababu ya mafuriko katika barabara na uwanja wa ndege wa Cairns, nao umelazimishwa kufungwa kwa sababu ya mafuriko, ndege zilizo kuwa zime egeshwa zikifunikwa kwa maji. Onyo za dharura za mafuriko, zimetolewa kwa eneo la Machans Beach, Holloways Beach, Yorkeys Knob na sehemu za Trinity Park, ambako wakaazi wame hamasishwa watafute sehemu salama. Waziri Mkuu Anthony Albanese amethibitisha kuwa majeshi yanaweza husika.

Idadi ya ajili barabarani nchini Australia imefika kiwango cha juu katika miaka mitano, hali ambayo imezua ombi kwa uwepo wa uwaji kuhusu data za ajali.
Kulingana na shirika la Australian Automobile Association, data muhimu kwa ubora wa barabara, sababu za ajali na utekelezaji wa sheria, kunaweza saidia kumaliza mwelekeo huu wa kutisha. Hata hivyo, shirika hilo la kilele linalo fuatilia vilabu vyama gari limesema, majimbo na wilaya hazijatoa taarifa yakutosha. Idadi ya watu 1,253 wame uawa katika barabara za Australia katika miezi 12 iliyopita. Takwimu hiyo inawakilisha 6.3% ya ongezeko kwa takwimu za mwaka jana pamoja na kiwango cha juu zaidi cha ajali za barabarani kila mwaka tangu Machi 2018. Jimbo la Kusini Australia lili rekodi ongezeko la juu la 61.4 katika vifo, ikifuatwa na jimbo la New South Wales ambalo lili rekodi 23.8% na jimbo la Victoria lilikuwa na 14.5%. Matukio yakusababisha vifo, yalipungua katika katika majimbo mengine yote pamoja na wilaya.

Jeshi la Israel IDF, limekiri kuwa asakri wake waliwaua kimakosa mateka watatu huko Gaza,licha ya kubeba fimbo ikiwa na bendera nyeupe kama ishara ya amani. IDF imesema askari walioua mateka hao walikiuka kanuni za vita. Mateka watatu wa Israel waliouawa kimakosa na vikosi vya jeshi la Israel, IDF, katika Ukanda wa Gaza walikuwa wamebeba fimbo iliyofungiwa kitambaa cheusi waakti wa tukio hilo, amesema msemaji wa jeshi la Israel, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, shirika la habari la Uhispania EFE na vyombo vya habari Israel. Tukio hilo lilitokea katika eneo la mapigano makali ambako wapiganaji wa Hamas wanaendesha operesheni zao katika nguo za kiraia na kutumia mbinu za ulaghai, alisema. Mateka hao walikuwa na umari wa miaka 25 hadi 28.

Serikali ya Kenya imejitenga na matamshi yaliyotolewa kwenye kikao cha waandishi wa habari mjini Nairobi na wanasiasa kadhaa wa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo (DRC) na makundi kadhaa yakiwemo kundi la waasi wa M23, kuwa wameunda vuguvugu jipya kwa jina la Muungano wa Mto Congo au Congo River Alliance. Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Jumapili Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Musalia Mudavadi, amesema kuwa serikali ya Kenya haikuhusika au haikujulishwa kuhusiana na kikao hicho kilichofanyika siku ya Ijumaa katika mji Mkuu wa Nairobi. Wakati huo huo kampeni za uchaguzi za DR Kongo zinakamilika rasmi leo wakati shirika la Human Rights Watch likitahadharisha kuwa ghasia zinazohusiana na uchaguzi zinatishia kuvuruga uchaguzi huo uliopangwa kufanyika mnamo siku ya Jumatano.

Na katika taarifa za michezo:
Timu mpya ya mchezo wa pete Melbourne Mavericks imethibitisha usajili wa mchezaji wakimatiafa wa Uingereza Eleanor Cardwell. Hii ni baada ya mchezaji huyo kusaidia timu ya Adelaide kushinda kombe la mwaka huu wa 2013. Cardwell, aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora katika fainali dhidi ya Swifts ya New South Wales, atajiunga na mwalimu wake wa zamani wa timu ya taifa Tracey Neville katika timu hiyo mpya. Timu ya Thunderbirds ilitangaza mnamo Septemba kuwa nyota huyo mwenye miaka 29, aliamua kuto cheza msimu wa pili katika klabu hiyo.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Taarifa ya Habari 18 Disemba 2023 | SBS Swahili