Waziri Mkuu Anthony Albanese amesema ana amini wa Australia watapiga kura ya Ndio katika kura ya maoni ya sauti yawa Australia wa kwanza, wanapo tafuta maboresho yamatokeo kwa wa Australia wa kwanza. Kauli hiyo imejiri wakati wakati tume ya uchaguzi ya Australia, ime chapisha kesi rasmi za kampeni za 'Ndio' na 'La' kwenye tovuti yake.
Wa Australia wanaweza endelea hisi maumivu ya ongezeko ya gharama ya umeme, kulingana na ripoti mpya ya shirika la sayansi lakitaifa la Australia. Ripoti ya shirika la Utafiti wa sayansi na viwanda la jumuiya ya madola almaarufu C-S-I-R-O, imeweka wazi kuwa uzalishaji wa gharama za umeme ume ongezeka kwa 20% kutoka mwaka uliopita.
Kikosi cha Afrika Mashariki kinachosimamia juhudi za kutafuta amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumatatu kimesema kitatuma tume ya uchunguzi katika eneo ambako wakazi waliwashutumu waasi wa M23 kuua watu 11. Kundi la M23 limekanusha kufanya mauaji hayo.
Mkutano mkubwa wa mwaka unaoangazia masuala ya uongozi na demokrasia na uliowashirikisha marais watatu wastaafu wa nchi za Afrika, pamoja na mambo mengine umesema demokrasia katika bara hilo ipo mashakani. Katika mkutano huo, wakuu hao wa nchi wastaafu pamoja na kueleza baadhi ya mafanikio ambayo nchi nyingi za Afrika zimefikia baada ya uhuru lakini wamekosoa mienendo ya utawalawa baadhi ya serikali za Afrika kwamba haizingatii utawala wa kisheria, demokrasia na ulinzi wa raia.
Watu wanane wakiwemo saba kutoka familia moja walifariki mjini Cairo Jumatatu wakati jengo la makazi katika mji mkuu wa Misri lilipoporomoka, ofisi ya mwendesha mashtaka na vyombo vya habari wamesema.