Kiongozi wa chama cha upinzani cha shirikisho anaihamasisha serikali itoe pendekezo la muswada kwa tume ya uadilifu yakitaifa. Mwanasheria mkuu Christian Porter amesema pendekezo hilo la muswada, kwa tume hiyo litatolewa hivi karibuni.
Waziri Mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern Jumamosi ameshinda uchaguzi mkuu kwa kishindo, kwa kupata ushindi wa waliowengi.
Maandamano yanatarajiwa kufanyika katika miji kadhaa nchini Ufaransa leo, kuonyesha mshikamano dhidi ya kisa cha kuchinjwa kwa mwalimu aliyewaonyesha wanafunzi vibonzo vya Mtume Mohammed. Kisa cha mwalimu huyo wa historia Samuel Paty kukatwa kichwa nje ya shule viungani mwa mji wa Paris Ijumaa iliyopita, kimeibua ghadhabu nchini Ufaransa na kukumbusha wimbi la machafuko ya Waislamu wenye itikadi kali ya mwaka 2015, ambayo pia yalichochewa na kuchapishwa kwa vibonzo vya Mtume Mohammed kwenye jarida la Charlie Hebdo.